wamuzi wa mchezo wa
hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Ngaya Club DE
Mbe ya Comoro, amewekwa hadharani na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Februari
12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Stade de Moroni uliopo katika Mji wa
Moroni nchini Comoro, utachezeshwa na mwamuzi wa kati raia wa
Shelisheli, James Fedrick Emile.
Caf ikiwa tayari imemtaja mwamuzi huyo
wa kati, lakini bado haijawaorodhesha wasaidizi wake ambao ni washika
vibendera wawili, mwamuzi wa mezani na msimamizi wa mchezo huo.
Baada ya mchezo huo, timu hizo
zitarudiana Februari 17, mwaka huu jijini Dar na mshindi wa jumla
atacheza hatua ya pili dhidi ya Zanaco ya Zambia au APR ya Rwanda.
Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania
Bara kwenye michuano hiyo, kwa sasa inaendelea na maandalizi makali
kuhakikisha inafanya vizuri huku ikiwa tayari imeanza harakati za chini
chini za kuwachunguza wapinzani wao hao.
0 maoni:
Chapisha Maoni