Pages

Alhamisi, 23 Februari 2017

Beyonce kughali kutumbuiza kwenye Coachella, mauzo ya tiketi yashuka




Beyonce, amelazimika kusitisha kwenda kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella Valley Music and Arts, mwaka huu.

Tangazo hilo limekuja miezi miwili kabla ya tamasha hilo kufanyika, April 15-17. Bey ameamua kuahirisha kutokana na kuwa mjamzito.

Muimbaji huyo mwenye ujauzito wa watoto mapacha, amelazimika kujiondoa kutokana na ushauri wa madaktari. Tangazo hilo limesababisha kushuka kwa mauzo ya tiketi kwa asilimia 12.
Coachella ndio tamasha linaloingiza fedha nyingi zaidi duniani. Mwaka jana liliingiza dola milioni 94.

0 maoni:

Chapisha Maoni