Baada ya kumwagana na Meek Mill mrembo Nicki Minaj amethibitisha ule msemo usemao ‘ukiona cha nini wenzio wanauliza watakipata lini’ kwani Drake ameonekana kwa mara ya kwanza akiwa na mrembo huyo tangia mwaka mmoja upite sasa.
Hiyo ilisababisha Drake kumfata Rais wa Young Money, Mack Maine na kuuliza kwa nini hakupewa taarifa kwamba familia ilikuwa pamoja tayari.
Kabla ya hapo, Nicki na Drake walikuwa hawasemeshani karibu miaka miwili tangu warekodi “Truffle Butter.” inadiwa kuwa Ex wa Nicki, Meek Mill ni moja ya sababu ya urafiki wao kufa, lakini kwa sasa Meek hayupo tena na Nick Minaj, yadaiwa YM Rappers kurudi tena.

Mbali na hilo tayari Nicki Minaj, Lil Wayne na Drake wako pamoja kwa sasa na tutegemee mazuri kutoka kwenye muungano huo.. Nicki alipost picha inayowaonyesha wapo pamoja huku wakionekana kuwa watu wenye furaha sana.

0 maoni:
Chapisha Maoni