MWENYEKITI wa Vikao vya Madiwani wa CCM, Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyemba amemaliza mvutano na mtafaruku wa madiwani wa chama hicho wa kususia vikao na kutoka nje kwa siku mbili mfululizo baada ya kukubali kuachia kiti na kumpisha Naibu Meya, Jumanne Ndege aweze kuviongoza.

Mwanyemba jana mchana alikubali kuachia kiti hicho baada ya madiwani kuendelea kuchachamaa na kutoka nje kwa siku ya pili, wakidai hawezi kuongoza kikao wakati mchakato wa kuchunguza tuhuma mbalimbali zikiwamo za ubadhirifu wa Sh milioni 30 unaendelea.
Anatuhumiwa kuhusika ka
tika ubadhirifu wa Sh milioni 30 za mradi wa maji katika Kata ya Zuzu ulioibuliwa na mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda, uliolenga kunufaisha wakazi wa kata hiyo, lakini utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kutokana na kugubikwa na ubadhirifu wa fedha za mradi huo.
Pia anatuhumiwa kutumia madaraka vibaya, kushiriki katika vitendo vya rushwa, kushindwa kutekeleza majukumu yake vizuri na kuwadanganya madiwani kwa makusudi pamoja na kupandikiza chuki za uongo miongoni mwao.
Katibu wa kikao hicho, Edward Maboje alipoulizwa kuhusu kuendelea kikao kwa siku ya pili huku baadhi ya madiwani wakiwa nje na Meya ameondoka, alisema mwafaka wa juzi haujafikiwa wa kumtaka meya asiongoze kikao pamoja na kutomalizika kwa ajenda, ndiyo maana kinaendelea.
Akizungumza baada ya kuachia kiti kwa N
aibu Meya, Mwanyemba alisema ameachia kiti ili kutumia muda vizuri kujibu barua ya Februari 20, mwaka huu iliyoandikwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi ya kujieleza ndani ya siku tano kuhusiana na tuhuma dhidi yake.
Sakata la kumkataa meya kuongoza vikao vya madiwani wa chama, ambaye ni mwenyekiti wao, liliibuka juzi baada ya madiwani 43 kati ya 47, kuorodhesha majina ya kutokuwa na imani naye na kumkataa asiongoze vikao vya chama hicho kwa sababu anatuhumiwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni