Na Alex Mwenda
Kiungo wa kimataifa wa timu ya Taifa Uganda ‘The Cranes’ Khalid Aucho
amejiunga na washindi wa Ligi ya Mabingwa 1990/1991 klabu ya Red Star
Belgrade ya nchini Serbia.
Aucho ambaye alikua kwenye michuano ya Mataifa Afrika (AFCON) Gabon
na kikosi cha Uganda, alitemwa mapema Januari 2017 na klabu yake ya
Baroka FC inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini pamoja na Geofrey
Massa.
Kabla ya kujiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini Agosti mwaka jana,
Aucho aliibukia Jinja Manispaa kabla ya kujiunga na Simba ya Uganda na
baadae kwenda Kenya kuzicheza klabu za Tusker na Gor Mahia FC.
Red Star Belgrade ndio pekee yenye mafanikio kutoka Ulaya Magharibi
kwa kufanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa, ikicheza fainali ya Kombe la
Mabingwa 1978 na mchezo wa UEFA Super Cup 1991.
Kufuatia Aucho kujiunga na klabu hiyo, kunafanya idadi ya wachezaji
wa Uganda wanaocheza nje ya nchi kuongezeka, kwani mpaka sasa ina
wachezaji zaidi ya 30 wanaocheza nje ya Uganda.
0 maoni:
Chapisha Maoni