Pages

Alhamisi, 23 Februari 2017

Mr NEY APEWA ONYO KALI NA MZEE WA UPAKO

Baada ya Rapa Nay wa Mitego kutangaza kuwa atafungua kanisa lake ambalo litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mungu aliye hai, Mchungaji maarufu nchini, Mchungaji Anthony Lusekelo amuonya kutomchezea Mungu. E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo.
Kupitia kipindi cha eNEWS cha EATV Mzee wa Upako aliulizwa kuzungumzia kauli ya Nay wa Mitego ya kutaka kuanzisha Kanisa lake alisema kanisa sio Biashara hivyo kama anafikiri hivyo atakuwa anamtania Mungu.

Kama unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili. Mungu hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu kufanya kanisa kama biashara. Baada ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto, Alisema Mch Antony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’.

0 maoni:

Chapisha Maoni