Mchezaji wa Chelsea Oscar
anatarajiwa kuwa mchezaji soka anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani
atakapohamia Ligi Kuu ya Uchina mwezi Januari.
Akifanikiwa kuondoka, basi Oscar, 25, ataungana na meneja wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ndiye mkufunzi wa Shanghai.
Taarifa zinasema atakuwa analipwa £400,000 kila wiki (£20.8m kila mwaka), ingawa huenda akapitwa haraka kwani kuna taarifa kwamba klabu za China zinajiandaa kulipa pesa nyingi kununua wachezaji wengine Januari. Mshahara wa Oscar ni sawa na £57,143 kila siku, au £2,381 kwa saa, au £39 kila dakika.
Kuna taarifa huenda Shanghai Shenhua ,ambao mkufunzi wao kwa sasa ni Gus Poyet aliyetoka Sunderland, wanapanga kumnunua nyota wa zamani wa Manchester United na Manchester City Carlos Tevez kutoka Boca Juniors. Tevez atakuwa analipwa £31.5m kila mwaka, sawa na £605,000 kila wiki.
LIST YA WACHEZAJI 10 WANALIPWA PESANYINGI DUNIANI
1) Oscar (Shanghai SIPG) £400,000 kila wiki £20.8m kila mwaka (kuanzia Januari)
2) Cristiano Ronaldo (Real Madrid) £365,000 kila wiki £19m kila mwaka (kabla ya kutozwa kodi)
3= Lionel Messi (Barcelona) £365,000 kila wiki £19m kila mwaka(kabla ya kutozwa kodi)
4) Gareth Bale (Real Madrid) £346,000 kila wiki £18m kila mwaka(kabla ya kutozwa kodi)
5) Hulk (Shanghai SIPG) £317,000 kila wiki £16.5m kila mwaka
6) Paul Pogba (Manchester United) £290,000 kila wiki £15m kila mwaka
7) Neymar (Barcelona) £289,000 kila wiki £15m kila mwaka(kabla ya kutozwa kodi)
8=) Graziano Pelle (Shandong Luneng) £260,000 kila wiki £13.5m kila mwaka
8=) Wayne Rooney (Manchester United) £260,000 kila wiki £13.5m kila mwaka
10) Zlatan Ibrahimovic (Manchester United) £250,000 kila wiki £13m kila mwaka
0 maoni:
Chapisha Maoni