Pages

Jumapili, 25 Desemba 2016

Ndege ya Urusi yatafutwa kwa nguvu zote

Urusi


Msako mkali unaendelea kutafuta miili ya askari wa Urusi walio waliokuwemo kwenye ndege iliyopata ajali kwenye bahari nyeusi iliyoanguka na kuua askri wote tisni na mbili waliokuwemo .

Wafanyakazi zaidi ya elfu tatu, wakiwemo wazamiaji zaidi ya elfu moja wako kwenye harakati za utafutaji manusura ama maiti za askari hao katika eneo la tukio.

Ndege iliyokuwa imebeba askari hao ilianguka dakika tatu baada ya kuanza safari kutoka katika mji wa Sochi ikiwa njiani kuelekea nchini Syria.

Abiria walio wengi walikuwa ni askari wa Urusi waliokuwa katika shamra shamra za sherehe za tamasha la kimuziki la Alexandrov wanaojulikana kama kwaya ya jeshi jekundu.

Ibada ya kuwaombea marehemu hao imefanyika mjini Sochi na miji mingine tofauti tofauti kabla ya siku maalumu ya Jumatatu iliyotangazwa kuwa ya maombolezo.

Mamlaka nchini Urusi zimetoa tamko kuwa zinafahamu fika wapi ilipo ndege hiyo katika bahari nyeusi.

Mpaka sasa miili saba ya askari imepatikana .Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kuwepo kwa manusura wa ajali hiyo.

Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini Urusi, Igor Konashenkov, amesema kwamba zoezi la utafutaji linaendelea.

0 maoni:

Chapisha Maoni