Pages

Jumamosi, 17 Desemba 2016

"NILILAZIMISHWA KUFANYA MAPENZI NA MWALIMU WANGU.....ALIPONIPA MIMBA ALIAMUA KUJIUA".....DENTI

Mwalimu ni kiungo muhimu sana katika malezi ya wanafunzi hapa nchini.Wao hushinda na watoto  wetu kutwa nzima .......
Kwa mantiki hiyo, tabia ya  mtoto yeyote aliyewahi kalia madawati  ina asilimia zaidi ya 70 ya tabia  za walimu wake......
Siku hizi mambo yamebadilika sana.Mwalimu wa miaka ya 90 ni tofauti kabisa na mwalimu wa miaka y leo.
Walimu wa leo wengi wao ni vijana wadogo ambao wengi wamejawa na tamaa za mapenzi.Wao hawajui kutongoza bali wanajua kulazimisha....
Inashangaza na  kusikitisha kuona walimu  wetu wakishindana  KUTOA BIKRA ZA WATOTO WA KIKE......Mtoto akikataa basi cha motoatakiona ....
Mtandao huu umebahatika kuongea na  mwanafunzi mmojaambaye ni mhanga wa tukio hilo la kulazimishwa mapenzi na mwalimu wake..........
HII NI  SIMULIZI YAKE:
 --------------------------------------------------------------------
"Mwalimu alianza kunitaka  tangu nikuwa  form one.Nilipomkataa alianza  kunichapa tena bila kosa maalumu na  kunipa adhabu kila  mara...
Baada ya kufanya hivyo kwa muda, aliamua kuniita ofisini na  kuniambia  kuwa  anatanisaidia  kimasomo endapo ntamkubalia.Niliamua  kumkubali kwa  kwa kuhofia  viboko na aliniambia  nisimwambie mtu.

Siku ya kwanza kufanya mapenzi alinipeleka gesti na aliniambia kuwa atatumia condom.Kwa kuwa  ilikuwa ni mara yangu  ya kwanza hatukuweza kutumia kinga na alifanya hivyohivyo.

Baada ya hapo tuliendelea  kufanya  hicho kitendo hata tukiwa shule.Wakati wa  kutawanyika, mwalimu alikuwa  akiniita  katika  ofisi yake  na  kunilazimisha tufanye.....

Miezi kadhaa baadaye, nilianza kujihisi tofauti na wazazi wangu waliyagundua mabadiliko hayo.Walinipeleka hospitali  na vipimo vilionesha kuwa  nna mimba.Waliponibana ilinibidi niwaeleze  ukweli.....

AFISA  ELIMU AINGILIA KATI:
Baada ya kubaini hali hiyo, baba  alinipeleka moja kwa moja mpaka kwa afisa elimu wa mkoa.Sikuwa na jinsi zaidi ya kueleza ukweli.Mwalimu aliitwa na kuhojiwa.Mwanzo alikataa kabisa lakini baada ya kubanwa ilibidi akubali.

Mwalimu alisimamishwa  kazi kwa muda  na  kufunguliwa mashitaka.Alikaa  polisi kwa  siku mbili, siku ya tatu alipata dhamana  akatoka.....

Alipotoka, mwalimu aliamua kujiua kwa sumu.Shule niliachishwa.nipo nyumbani na mtoto.
--------------------------------------------------------------------
MTAZAMO WETU:
Ni ukweli usiopingika kuwa walimu wa siku hizi wamekuwa ni kero kwa watoto wa kike.Walimu hao  hutumia  viboko  kama msingi wa kuwafanya  wakubaliwe maombi yao.Hii  ni changamoto  kubwa  sana inayotukabili sisi wazazi.

Nadhani huu  ni wakati mwafaka kwa  wanafuni kujitambua  na  kutokuwa wasiri kwa  kuhofia  kuchapwa viboko.Waeleze  wazazi  wako juu  ya  mkasa unaokukabili  maana hayo ndo maisha yako  ya baadaye

0 maoni:

Chapisha Maoni