Mwandishi Alex Mwenda
Mahusiano ni suala tata sana kuliko hata kutafuta pesa, pesa ni rahisi
sana kuzitafuta panapo utulivu wa ubongo na pasipokuwa na mgogoro wa
nafsi.
Wanawake siku zote huuliza, "Nitajuaje kama huyu ni mwanaume bora kwangu na aliye ndoto ya maisha yangu?"
Jibu langu siku zote litakuwa hili, wanaume hutofautiana sana kutokana
na malezi waliyopitia, aina ya maisha, influence ya marafiki, etc.
Hata hivyo kuna mambo ya kawaida ambayo kama mwanaume uliyenae hayatimilizi, kunaweza kuwa na tatizo.
1. Mwanaume bora huihudumua familia yake, mwanaume ambae hata kuhudumia
familia ni mtihani hilo ni tatzo, mwanaume ambae hata kumnunulia
mwanamke wake mafuta, nguo, viatu au kitu chochote kidogo hawezi huyo
hawezi kuwa bora.
2. Mwanaume aliye sahihi kwako hukufanya wewe mwanamke uwe bora, hukupatia maono yake, hukueleza ndoto zake, hupata tabu sana endapo utakua katika hali ya sintofahamu.
3. Mwanaume asiye bora kwako, huwa mpole tu pale anapotaka kufanya mapenzi na wewe, ikifika hatua hii hujishusha na siku hiyo hua karibu na wewe sana, na baada ya kufanikisha hurudi katika hali yake ya kawaida mpaka msimu mwingine wa Sex unapokaribia. Sex pekee haiwezi kujenga Ndoa.
4. Mwanaume asiye sahihi kwako hawezi kukueleza mipango yake, hana Mungu ndani yake, anathamini marafiki zake zaidi yako, huthimini pombe kuliko kitu chochote.
5. Hawezi kukuchukua na kukupeleka Lodge au ghetto kwake tu, b
ali hukupeleka na kukutambulisha kwa wazazi wake, ndugu na marafiki, ukiona hataki kukutambulisha hapo shtuka, anapitisha muda tu kwako.
6. Siku zote Hatakumbuka ni lini Period yako inaanza na itakua kwa muda gani pekee bali atakumbuka pia siku yako ya kuzaliwa, na kukumbusha mipango ambayo mmeipanga ili muweze kuitumiza.
7. Hatakukumbusha ni lini mnatakiwa kukutana kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa bali pia atakukumbusha kusali na kufunga ili muweze kurithi kwa pamoja ufalme wa Mungu.
Unahitaji mwanaume mwenye mawazo ya kina, mwanaume mwenye hofu ya Mungu, Mwanaume anaeweza kukupa kitu fulani katika maisha yako mbali na kukaa lisaa limoja kwenye tendo la ndoa.
Hata hivyo baadhi ya wanaume wasio na hofu ya Mungu hu 'pretend' baadhi ya mambo alimradi ampate mwanamke na kuzini nae, Ni vema na busara mwanamke akawa na Mungu ili Mwanaume amtafute kwanza Mungu ndipo awe na wewe.
"A real man can't stand seeing his woman hurt. He is careful with his decision and actions, so he never has to be responsible for her pain."
Image may contain: 2 people, people sitting and indoor

0 maoni:
Chapisha Maoni