Kaka huyu aliingia ndani huku kijasho kikimteremka mithili ya mtu
aliyekuwa anakimbia. Dada huyu alimkaribisha vizuri, yule kaka aliomba
maji ya kunywa huku muda wote akimtizama kwa umakini dada huyu mrembo,
aliyeumbika kila idara na ile kanga nyepesi aliyovaa ilikuwa ikionyesha
umbo zuri la dada huyu ambaye waswahili huwa wanasema, mtoto kajaaliwa
(mashalaah) Kaka alikuwa akivuta pumzi kwa haraka haraka, na kusema
"Nimefurahi sana, umenikaribisha nyumbani kwako ni pazuri sana." Yule
dada alitabasamu na kusema "Asante sana, nimefurahi pia umeitikia wito
wangu, samahani kwa usumbufu wangu".
Yule kaka alitabasamu huku akijisogeza sogeza "Hakuna tatizo, usijali
kabisa, mimi nipo kwa ajili yako, naimani sasa nina...." Kabla
hajamilizia kuongea yule dada alimshika mikono yake miwili huku
akimtizama machoni, kwa macho yake malegevu, mithili ya mtu aliyekula
kungu "Samahani kaka, mimi nimekuita hapa kuna jambo nataka unishauri,
nataka kujua ni zawadi gani nzuri unaweza kumpatia mwanaume unayempenda"
Kaka yule alikuwa akitetemeka na kusema
"Chochote tu, zawadi ni zawadi,
alimradi kuwe na mapenzi ya kweli" Dada yule alitabasamu na kusema "Ni
kweli, mapenzi ya kweli ndiyo jambo la msingi, nitampenda maisha yangu
yote" Kaka yule akauliza "Utampenda? Nani huyo"
.
Yule dada alitabasamu tena na kusema "Samahani, rafiki nilikuwa
sijakuambia, wiki ijayo nafunga ndoa na mpenzi wangu wa muda mrefu
ambaye nampenda sana, na pia nilikuita ili nikupe kadi ya harusi,
nitafurahi kukuona, kwani wewe ni rafiki yangu pia" Yule kaka alibaki
amepigwa na butwaa, "Ati, nini unaolewa, daaah, jamani, kwahiyo."
Alinyanyuka na kuondoka bila ya kuaga huku akimuacha yule dada anamuita
ili ampatie kadi bila ya mafanikio.
0 maoni:
Chapisha Maoni