Pages

Jumanne, 28 Februari 2017

BATULI AMPINGA WEMA, ‘WASANII TULIOSHIRIKI KAMPENI ZA CCM TULILIPWA NA MIKATABA IPO’

Msanii wa Filamu nchini, Batuli aliyeshiriki kampeni ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya ‘Mama ongea na Mwanao’ amekanusha taarifa zinazoeleza kuwa wasanii walioshiriki kampeni hiyo hawakulipwa.Batuli amesema taarifa hizo siyo za kweli na kueleza kuwa CCM iliwalipa wasanii wote walioshiriki katika kampeni ya ‘Mama Ongea na Mwanao’ na mikataba ya malipo hayo ipo.

 Nakanusha  za kwamba wasanii tulioshiriki kampeni za CCM ‘Mama ongea na mwanao’ hatukulipwa, tulilipwa na mikataba ipo” amesema Batuli
 Batuli amesema hayo leo Februari 28, 2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari, kufuatia taarifa ya msanii wa filamu, Wema Sepetu kuwa wanaidai CCM fedha za kampeni. Wema alinukuliwa akiongea hayo wakati akitangaza kujiengua katika chama hicho na kuhamia Chadema.
 Batuli amesema kuwa haiwezekani msanii mkubwa hivyo asema hakulipwa wakati yeye ndio alikuwa anawalipa wasanii wengine.Haiwezekani wewe staa mkubwa unasema haujalipwa, wakati wewe ndio ulikuwa unalipa watu” amesema Batuli

0 maoni:

Chapisha Maoni