Na Alex Mwenda
Klabu
ya Yanga imekataa kuilipa Simba fidia ya Sh milioni 50 kuhusu ishu ya
Hassan Kessy hivyo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inatarajia kukutana kwa mara nyingine
kupitia upya shauri hilo.
Kamati
hiyo iliitia hatiani Yanga kwa kosa la kumsajili Kessy ambaye alikuwa
akichezea Simba akiwa ndani ya mkataba kwa kutakiwa kulipa fidia ya Sh
milioni 50 kwa Wekundu wa Msimbazi.
Akizungumza
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucus alisema: “Tumepokea barua kutoka
Yanga ikitaka suala lao lijadiliwe upya, hivyo kamati hiyo inatarajia
kukaa wakati wowote kuanzia sasa ili kujadili suala hilo.
“Yanga
wamefikisha barua ya kupinga adhabu wanataka hukumu hiyo ipitiwe upya
hivyo kamati itakaa wakati wowote kuanzia sasa japokuwa hatujui kama
itatenguliwa ama la.”
Aidha,
alipotafutwa Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele kuzungumzia suala
hilo, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi
wa simu hakujibu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, naye simu yake iliita bila kupokelewa.
0 maoni:
Chapisha Maoni