Na Alex Mwenda
Aliyekuwa
Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface
Mkwasa
analidai Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Sh milioni 80 ikiwa ni fedha za
malipo ya mshahara wake ambazo hajalipwa kwa miezi kadhaa.
TFF
imeamua kuachana na Mkwasa hivi karibuni kwa makubaliano kufuatia mkataba wake
kutarajia kufikia tamati Machi, mwaka huu kisha kumteua Salum Mayanga kushika
nafasi yake hiyo.
Mayanga
aliyekuwa akiifundisha Mtibwa Sugar, ana jukumu la kuandaa kikosi
kitakachowania kufuzu Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan) Aprili
mwaka huu.
Mshahara
wa Mkwasa kwa mwezi ulikuwa Sh milioni 28 ambao aliurithi kutoka kwa Mart Nooij
ambaye alisitishiwa mkataba kutokana na TFF kutoridhishwa na utendaji wake.
Akizungumza, bosi
mmoja wa TFF alisema, Mkwasa anadai Sh milioni 80 ambazo anatarajiwa kulipwa
kwa mikupuo miwili ndani ya mwezi huu.
“Ni
kweli Mkwasa anaidai TFF Sh milioni 80 ambazo zinatokana na malipo ya mshahara
wake ambao ulikuwa ukilimbikizwa, hivyo TFF ipo katika hatua za kumlipa fedha
zake hizo kabla ya kocha mpya kuanza kazi.
0 maoni:
Chapisha Maoni