By Alex Mwenda
Kliniki
ya soka ya Airtel Rising Stars iyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa
inatarajiwa kuanza Jumatatu, Januari 16 kwenye Uwanja wa Karume huku
wavulana 40 na wasichana 25 waliofanya vyema kwenye michuano ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 wakishiriki.
Kufanyika kwa kliniki hiyo kutakuwa ni hitimisho ya michuano ya Airtel Rising Stars msimu wa sita.
Kliniki
hiyo itakuwa ya siku sita na itaendeshwa na makocha wa timu ya soka ya
taifa Oscar Milambo akisaidiwa na Kim Paulsen kwa wavulana huku
wasichana wakifundishwa na Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Queens, Sebastian
Nkoma.
Akizungumzia
maandalizi ya kliniki hiyo, Mwenyekiti wa Maendeleo ya soka la vijana
kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi
alisema, “Kliniki hiyo itatoa fursa kwa vijana kujifunza mbinu mpya za
mpira, na kupata mafunzo kutoka kwa makocha wazoefu ili kuongezewa
vipaji vyao.
“Sisi
TFF tumefanya maandalizi yote ya kliniki na tumeichukua kwa uzito wa
hali ya juu kwa kuwa ndio njia sahihi ya kupata wachezaji wa timu zetu
za taifa, Serengeti Boys na Taifa Queens.” alisema Nyenzi na kuongeza:
“Tunaamini
ya kwamba kliniki haitakuwa na mafanikio kwa wachezaji tu bali na timu
zetu kupata wachezaji walio bora. Tumekuwa tukishuhudia wachezaji wazuri
wenye vipaji kwenye kila msimu wa Airtel Rising Stars. Nachukua nafasi
hii kuzishauri klabu zetu za mpira wa miguu kujitokeza kuangalia
wachezaji wakati wa siku sita za kliniki hii ya Airtel Rising Stars.”

Kwa
upande wake, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini wa umri wa
miaka 15, Oscar Milambo alisema: “Wachezaji watafundishwa nidhamu ya
mpira, ndani na nje ya uwanja, jinsi kumiliki mpira mbele ya mchezaji wa
timu pinzani, kutoa pasi za uhakika pamoja na mafunzo ya nadharia.”
Sambamba
na hayo wachezaji pia watakuwa na fursa ya kukutana na wenzao na hii
itakuwa na hamasa kwao kwani wengi wao itakuwa mara ya kwanza kupata
mafunzo kutoka kwa makocha. Milambo aliongeza kuwa vijana hao
watafundishwa jinsi mchezaji anavyotakiwa kujitunza kwa manufaa ya
kuendelea kutunza kipaji chake.
Akizungumza
juu ya kliniki hiyo, Ofisa Uhusiano Airtel Tanzania, Jane Matinde
alisema michuano ya Airtel Rising Stars 2016 imekuwa na mafanikio
makubwa na kuwa kufanyika kwa kliniki kutahitimisha Airtel Rising Stars
msimu wa sita na kufungua pazia kwa maandalizi ya Airtel Rising Stars
msimu wa saba.
Michuano
ya Airtel Rising Stars mwaka 2016 tuliunganisha na promosheni ya
kampuni ya Airtel ya ‘Airtel Fursa’ ambayo ni maalum kwa kuwawezesha
vijana kufanikisha malengo yao.
Matinde
aliongeza kuwa Airtel inajivunia kuwa sehemu ya mradi huu wa kukuza
vipaji vya soka kwani imesaidia kubadilisha soka la Tanzania. Airtel
Rising Stars inalenga kutafuta vipaji chipukuzi kuanzia ngazi ya chini
mpaka ngazi ya Taifa.
“Kampeni
yetu ya Airtel Fursa inalenga kuwainua vijana na kuwawezesha kufikia
ndoto zao inaenda sambamba na program hii ya Airtel Rising Stars na
tunajisikia furaha kuendelea kuwafikia vijana katika nyanja mbalimbali,”
aliongeza Matinde.
Wachezaji
zaidi ya 1000 wavulana na wasichana walishiriki kwenye michuano ya
Airtel Rising Stars 2016 kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya,
Arusha, Kinondoni, Ilala, Temeke,Lindi na Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni