Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa Edward Lowassa,amewaomba marais
wastaafu kuingilia kati siasa za chuki alizozisema zimeanza kujitokeza
nchini.
Ameyasema hayo wakati akifunga Kampeni za Udiwani ktika kata ya
Isagenhe wilayani kahama mkoani shinyanga,alipomnadi mgombea udiwani wa
kata hiyo kupitia Chadema Richard Luziga,amesema kuwa kadri siku
zinavyokwenda baadhi ya watu wameanza kuendesha siasa za chuki huku
wengine wakimtabiria kifo.
“Hizi chuki ni mbaya sana wanazielekeza kwa watu na kuzifanya ziwe
mbaya zaidi,kwa mfano wapo walionitabiria kifo,lakini Mwenyezi Mungu
amewatanguliza mbele ya haki kabla yangu,nasema siasa za chuki
hazitusaidii kitu katika nchi hii, ni vizuri tujenge umoja na mshikamano
katika nchi yetu,”amesema Lowassa.
Aidha, kwa upande wake kada wa chama hicho,Khamis Mgeja aliyewahi
kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa shinyanga,amewataka wakazi wa kata ya
Isagenhe kumchagua mgombea wa chma hicho.
Kwa upande wake Mgombea udiwani wa Chadema Richard Luziga,amewaomba
wananchi wamchague kwa kura nyingi na kwamba iwapo atashinda,mambo
takayoyapa kipaumbele katika kuyashughulikia ni ujenzi wazahanati, umeme
na kufikisha maji katika kata hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni