Mashabiki
wa klabu ya Arsenal wamemuangukia mshambuliaji Alexis Sanchez kwa
kumtaka asichukue maamuzi ya kuondoka klabuni hapo, baada ya kuandika
ujumbe mzito kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mashabiki
wa Arsenal wanaomfollow mshambuliaji huyo, walionyesha kushtushwa na
ujumbe uliandikwa na Sanchez katika ukurasa wake, ambao unasomeka “Watu
wazito wanacheka huku wakiwa wamevunjika moyo. Wanalia huku milango
ikiwa imefungwa na wanapigana bila ya muhisika kuwajali.”
Mashabiki
wa Sanchez kwa nyakati tofauti walitoa maoni yao kuhusu ujumbe huo, na
wengi wao walionyesha hisia ya kuguswa na maneno alioyaandika
mshambuliaji huyo.
Asilimia
kubwa ya mashabiki, walimtaka asifanye maamuzi magumu ya kuondoka
klabuni hapo, na badala yake aendelee kuwatumikia hadi watakapofikia
hatua ya kufurahia mataji.
Mshambuliaji
huyo amewaweka mashabiki wa Arsenal katika hali ya sintofahamu kuhusu
uhusiano wake na Arsenal Wenger, ambapo zaidi ya mara moja amekua
akionyesha vitendo vinavyopingana na mzee huyo.
Sanchez
alionyesha unyonge baada ya kutolewa nje ya uwanja wakati wa mchezo wa
mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Arsenal walipambana na Swansea city
na kuchomoza na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.
0 maoni:
Chapisha Maoni