Na Alex Mwenda
Serikali imejipanga kupitia upya kanuni za utangazaji za Sheria ya
Utangazaji ya mwaka 2003 ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Moses Nnauye wakati wa ziara yake kwa vyombo vya habari vya Channel, na
Tumain Media iliyolenga kuimarisha mahusiano yaliyopo kati ya Serikali
na vyombo vya habari nchini.
Nape amesema kuwa lengo la mapitio ya kanuni hizo ni uboreshwaji wa kanuni hizo ili kuisaidia kukuza sekta ya utangazaji.
“Kuna baadhi ya wadau wamekuwa wakilalamika kuhusu kupitwa kwa wakati
kwa kanuni hizo, hivyo tumeona ni vyema kuungana nao ili kuzipitia upya
na kuona palipo na mapungufu” amesema Nape.
Aidha, Nape ameongeza kuwa baadhi ya maeneo katika kanuni hizo
yanayohitaji kupitiwa upya ni aina za leseni zilizopo, kubadilika kwa
jamii inayotuzunguka pamoja na mabadiliko ya teknolojia yanayokuwa kwa
kasi.
Mbali na hayo Nape amesema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano
Tanzania (TCRA) ipo katika hatua za mwisho za kuandaa kanuni za
kudhibiti masuala ya matumizi ya mitandao ya kijamii nchini.
Katika hatua hiyo Waziri Nape amewataka wadau mbalimbali kutoa maoni
ili kusaidia kuboresha kanuni za mitandao ya kijamii kwa lengo ili
kukuza tasnia ya habari.
0 maoni:
Chapisha Maoni