Jumamosi dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Amesema tatizo la ubutu wa ushambuliaji ndio limeifanya Simba wapoteze dhidi ya Azam FC.
Moloto alisema kuwa Simba ilizinduka katika kipindi cha pili baada ya kuingia kwa Mavugo, Ajibu na Kichuya. Kocha huyo wa zamani wa Simba alisema kuwa bado Simba ina nafasi ya kufanya vizuri endapo itabadilisha aina ya mchezo wake.
“Huwezi kufunga kwa kutumia winga peke yake, iliamka katika dakika 10 za mwisho lakini ilikuwa wamechelewa,” alisema Mkurugenzi huyo wa ufundi wa mabingwa wa Afrika.
Alisema kwa kuwa bado anaipenda Simba na akipata nafasi atalishauri benchi la ufundi.
Moloto aliwahi kuifundisha Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa msimu mmoja.
Moloto amekuja nchini huku na mabingwa hao kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Simba Jumatano na Yanga Ijumaa kusapoti kampeni ya vita dhidi ya mauaji ya tembo.
0 maoni:
Chapisha Maoni