NA Alex Mwenda
Raundi ya tano ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam
2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), utaanza Jamamosi Januari
21, 2017 kwa timu za Majimaji na Mighty Elephant za Songea kucheza
kwenye Uwanja Majimaji mjini Songea.
Ratiba ya ASFC inaonesha kwamba timu za Alliance na Mbao za Mwanza
zitacheza pia keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati
Young Africans itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini
Dar es Salaam.
Jumapili Januari 22, mwaka huu Ruvu Shooting itacheza na Kiluvya
United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati
Toto Africans itacheza na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza huku Simba itakipiga na Polisi Dar kwenye Uwanja
wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kadhalika Mbeya Warriors ikicheza na
Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Jumatatu Januari 23, mwaka huu Stand United itacheza na Polisi Mara
kwenye Uwanja wa Karume Mara wakati Azam itacheza na Cosmopolitan kwenye
Uwanja wa Chamazi wakati Ndanda itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona.
Jumanne Januari 24, mwaka huu Mtibwa Sugar itacheza na Polisi Moro
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Kurugenzi ya Iringa
itacheza na JKT Ruvu huko Mafinga huku Mbeya City ikipangwa kucheza na
Kabela City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ilihali Madini na Panone
zitacheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Januari 25, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na
Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mchezo
mwingine utakaozikutanisha timu za African Lyon na Mshikamano utapangiwa
tarehe mpya. Mechi hiyo imepangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru.
0 maoni:
Chapisha Maoni