MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana usiku
amefunga bao lake la 11 tangu ajiunge na KRC Genk ya Ubelgiji.
Samatta
alifunga bao hilo katika ushindi wa 3-0nyumbani Uwanja wa Luminus Arena
dhidi ya KV Kortrijk kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Nahodha
huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, ijulikanayo kama Taifa Stars kwa
jina la utani, alifunga bao hilo dakika ya 42 likiwa la pili kwa Genk
akimalizia pasi ya Siebe Schrijvers.
Mabao mengine ya Genk yalifungwa na Schrijvers dakika ya nne na Alejandro Melero Pozuelo dakika ya 68.
Samatta alitolewa dakika ya 87 baada ya kazi nzuri jana
Huo ulikuwa mchezo wa 38 kwa Samatta tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 20 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 19 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na nane msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati tisa hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 11, matano msimu huu na sita msimu uliopita.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot/Jackers dk19, Castagne, Dewaest, Colley, Uronen, Heynen, Malinovskyi/Berge dk68, Pozuelo, Trossard, Authors na Samatta/Naranjo dk87.
KV Kortrijk: Sifakis, Goutas, Saadi, Van Der Bruggen/Kage dk68, Gigot, Joãozinho, Rougeaux, Rolland, Ouali/Mercier dk87, D'Haene na Sarr/Chevalier dk45.
0 maoni:
Chapisha Maoni