Klabu ya Tottenham imefutilia mbali ndoto ya Chelsea kutaka kuweka
historia katika ligi kuu ya England kwa kushinda michezo 14 baada ya
vinara hao kufungwa 2-0 White Hart Lane.
Spurs wamesogea mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi baada ya
mchezaji Dele Alli kufunga magoli yote mawili kwa njia ya kichwa hii
ikiwa ni mwishoni mwa kipindi cha kwanza na dakika ya 54.
Alli alifunga vyema kwa kupokea pasi safi kutoka kwa Christian Eriksen kwa magoli yote mawili.
Eden Hazard alikosa nafasi mbili za kuiokoa Chelsea lakini Spurs
waliweza kufanikiwa kaupata point tatu muhimu na kuwaondoa majirani zao
Arsenal katika nafasi ya nne.
0 maoni:
Chapisha Maoni