Mwaka 2017 umeanza vibaya kwa Chris Brown na Soulja Boy – kwakuwa wameanzisha bifu chanzo kikiwa ni mrembo Karrueche Tran.
Bifu ya Chris Brown na Soulja Boy inayoendelea imemkera Karruache
Tran na ameamua kufunguka. Wasanii hao wameendelea kutupiana vijembe
kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuingia ugomvi ambao Karruache
aliyekuwa mpenzi wa Breezy anahusishwa.
Tangu alipoachana na Karrueche Chris amekuwa akimfuatilia mrembo huyo
huku mara kadhaa akigombana na wanaume ambao wanaomtolea udenda. Na
sasa balaa limemkumba rapper Soulja Boy baada ya kulike picha ya mrembo
huyo kwenye mtandao wa Instagram kitendo ambacho kimeonekana kumkera
Brown.
Mrembo huyo ameiita drama ya wasanii hao kuwa ni ya kijinga na haina
maana yoyote hata katika mwaka mpya. Amewaomba wamtoe kwenye malumbano
yao.
Tazama alichokiandika pamoja na jibu la Chris Brown..

Hii
inshu yote ilikuja baada ya Soulja Boy kufunguka kupitia mtandao wa
Twitter kuwa Chris amemtafuta na kumpiga mikwara baada ya kulike picha
hiyo.

Chris Brown amekuwa akijaribu mara kadhaa kutaka kurudiana na Karrueche lakini imekuwa ngumu kwa mrembo huyo kukubali.
0 maoni:
Chapisha Maoni