Aliyekuwa Rais wa muda mrefu wa Gambia, Yahya Jammeh ameondoka nchini
humo Jumamosi usiku na kwenda nchini Equatorial Guinea baada ya
kushindwa uchaguzi na kugomea kuondoka madarakani hali ambayo ilizifanya
nchi za jirani kutumia diplomasia kumuondoa madarakani.
Jammeh amedaiwa kuondoka na mali za mamilioni ya pesa pamoja na magari ya kifahari.
Mshauri maalumu wa Rais wa Gambia
Adama Barrow amesema zaidi ya dola za Kimarekani milioni 11 zinaaminika
kutoweka katika hazina ya serikali, kufuatia kuondoka madarakani kwa
mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh.
Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.
Kwa sasa Rais Barrow amekuwa akifanya kazi na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha na wengine kutoka Benki kuu ya nchi hiyo kupata kiasi halisi kilichopo.
Habari zinasema magari ya kifahari na mali nyingine zilionekana zikipakiwa katika ndege ya mizigo ya Chad kwa niaba ya Rais Jammeh siku alipoondoka nchini humo.
Maelfu ya watu walikusanyika katika Ikulu ya nchi hiyo jana jioni wakiyaangalia majeshi ya Senegal yakiingia kwa ajili ya kuweka usalama kabla ya kurejea nchini kwa Adama Barrow.

alisema atarejea tu baada ya kuhakikishiwa usalama wake.
0 maoni:
Chapisha Maoni