Mtengeneza sanamu maarufu mjini Las Angels nchini Marekani ‘Ginger’ ametengeneza sanamu ya Kanye West iliyofananisha na picha ya Yesu Kristo.
Msanii huyo aliyetengeneza sanamu amesema sababu za kutengeneza sanamu hiyo ni kumfariji Rapa Kanye West kwa matatizo aliyopitia mwanzoni mwa mwaka huu kama Kulazwa hospitalini kwa matatizo ya akili,baada ya kumpa ushirikiano rais Donald Trump na kupondwa vikali na watu weusi kwa kukutana na Donald Trump.

Sanamu hii ni ya Plastic na mtengenezaji huyo amesema sababu zingine ni Kutoa sifa kwa Kanye West kama Producer na mwandishi bora wa mashairi huku akiwaonya watu kuwa Kanye West sio Mungu mpaka alipopata matatizo ndipo kila mtu akaanza kumtukana na kumkejeli,kwani ni sawa na kama walimuweka kwenye msalaba.
0 maoni:
Chapisha Maoni