Pages

Jumanne, 1 Agosti 2017

Waziri Mkuu awaandalia chakula SIMBA wenye njaa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya, Emanuel Kiabo kumkamata na kumuhoji aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya Atanas Kapunga na wenzake 11 kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 63.448.
Image result for waziri mkuu majaliwa
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Jumatatu hii alipozungumza na watumishi wa Halmashauri za wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Benjamin Mkapa.
“Serikali hii haiwezi ikawaacha watu hawa ambao wameisababishia hasara kubwa kiasi hiki tena kwa halmashauri moja. Kama wako humu ndani naagiza wakamatwe na waanze kuhojiwa na ambao wamestaafu au kuhamishwa kituo cha kazi wasakwe popote walipo ili nao waje kuhojiwa,” aliagiza Waziri Majaliwa.
Wengine ni waliowahi kuwa wakurugenzi wa Jiji hilo ambao ni Bw. Mussa Zungiza, Bi. Elizabeth Munuo, Bw. Juma Idd na Dkt. Samwel Lazaro aliyekuwa akikaimu nafasi ya Ukurugenzi.
Aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji, Bw. James Jorojik pamoja na waliokuwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ambao ni Bw. Mussa Mapunda, Bw. Samweli Bubengwa, Bw. Davis Mbembela, Bi. Lydia Herbert na Bw. Bernard Nsolo ambao walipitisha nyongeza ya mradi huo bila ya kuzingatia maslahi ya Jiji pamoja Emily Maganga ambaye hakuishauri vizuri bodi hiyo.
Waziri Mkuu amesema watumishi hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria kwa kuwa wameisababishia serikali harasa kubwa katika mradi wa ujenzi wa soko la Mwanjelwa Jijini Mbeya ambalo hadi sasa halijaonyesha tija.

Jumatatu, 29 Mei 2017

Foby ajiweka kando ya Diamond na Ali Kiba, amvuta Lady Jay Dee

Na Alexx Mwenda
Nyota mpya anayeng’ara kwenye anga ya Bongo Flava, Foby amefunguka yanamhusu akiwaweka kwenye sentensi zake, Diamond, Ali Kiba na malkia wa muziki huo nchini, Lady Jay Dee.Image result for FOBY ONE

Mkali huyo wa ‘Star’ na ‘Ila’ amesema amefunguka katika mahojiano aliyofanya na Dar24 hivi karibuni, ambapo ameeleza kuhusu safari yake ya muziki, utunzi wa nyimbo zake pamoja na namna anavyoweza kuwaandikia mashairi wasanii wengine.
Tofauti na wasanii wengi, Foby ambaye amedai kuwa amekuwa akiandika ngoma nyingi za wasanii wakubwa licha ya kutopewa haki ya sifa stahiki, hivi sasa ameamua kuwa kwa kila wimbo mmoja anaoandika atalipwa shilingi laki tano.
Katika hatua nyingine, msanii huyo amezungumzia kile ambacho baadhi wamekuwa wakikizungumza kutaka kumfananisha na mafahari wa Bongo Flava, Ali Kiba na Diamond huku akimtaja Lady Jay Dee kwenye hoja ya mwanamuziki wa kike anayemkubali zaidi.

BAADAY MIAKA 45, TIMU HII YAREJEA LIGI KUU ENGLAND



Wachezaji wa Huddersfield Town wakishangilia na taji lao la mechi ya mchujo ya Championship kuwania kupanda Ligi Kuu England baada ya ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 leo Uwanja wa Wembley,

 London. Liam Moore alipaisha mkwaju wake kabla ya Danny Ward kuokoa penalti ya Jordan Obita na pamoja na kipa Ali Al-Habsi kuokoa tuta la Michael Hefele, haikuzuia Huddersfield Town kurejea Ligi Kuu mwa mara ya kwanza tangu mwaka 1972 

SHABIKI WA SIMBA ALIEPATA AJARI NA KUFARIKI KUZIKWA ARUSHA

Na Alexx Mwenda
MWILI wa marehemu Shose Fidels Alhamisi utasafirishwa kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yaatakayofanyika Ijumaa.
Taarifa ya familia ya marehemu imesema kwamba mwili wa mpendwa wao, Shose utaagwa mapema Alhamisi kabla ya safari ya kuelekea Moshi tayari kwa maishi yake Ijumaa, ambayo yatafanyiak Uru.

Shose alifariki dunia Jumapili mchana, muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, kufuatia ajali ya gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Shose Fidels atasafirishwa Alhamisi ukwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yaatakayofanyika Ijumaa

Binti huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 na ushei, alikuwa pamoja na Nahodha wa Simba, Jonas Mkude kwenye gari hilo na watu wengine, wakitokea Dodoma, ambako jana timu yao ilitwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Jamhuri.

Ndani ya gari hilo walikuwepo pia wapenzi wengine wa Simba, Jasmin na Faudhia ambao wameumia na wamelazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro na hali zao zinaendelea kuimarika.
Hii ndiyo gari iliyochukua uhai wa Shose (picha ndogo juu kulia)

Mkude alirejeshwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi katika hospitali ya Muhimbili kabla ya mapema Jumatatu kuruhusiwa, wakati dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la utani, Rais wa Kibamba anaisaidia Polisi.

KOCHA MPYA WA BARCELONA AWEKWA HADHARANI

Na Alexx Mwenda
KLABU ya Barcelona imemtangaza Ernesto Valverde kuwa kocha wao mpya, mtu mzima huyo wa umri wa miaka 53 akisaini mkataba wa miaka miwili.

Rais wa klabu, Josep Maria Bartomeu ametangaza uteuzi wa kocha huyo mpya katika mkutano na waandishi wa habari leo, ikiwa ni siku mbili baada ya Luis Enrique, aliyeshinda mataji tisa kati ya 13 ndani ya misimu mitatu kuondoka kwenye klabu hiyo.

Valverde atatambulishwa rasmi Alhamisi. Bartomeu amesema: "Nimezungumza naye leo amefurahi sana kwa sababu na changamoto maalum sana kwake. Anastahili, kwa kujua na kwa uzoefu alionao,".

Ernesto Valverde anarithi nyayo za Luis Enrique kwa kuwa kocha mpya wa vigogo wa La Liga, Barcelona   PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

Valverde anafuata nyayo za Pep Guardiola, Tito Vilanova na Luis Enrique ambao kwanza walianza kama wachezaji wa klabu hiyo kabla ya kuwa makocha.

Wote walishinda mataji ya Ligi katika misimu yao ya kwanza na jukumu la kwanza la Valverde kuwarejeshea Barcelona taji hilo baada yaa msimu huu kuchukuliwa na Real Madrid.

Atakuwa na muda mfupi sana kabla ya kumenyana na Real Madrid mara tatu – kwanza kwenye ziara ya klabu ya kujiandaa na msimu mpya na baadaye mara mbili kwenye Super Cup ya Hispania nyumbani na ugenini.

Valverde aliichezea Barcelona kwa miaka miwili, kuanzia 1998 hadi 2000 akicheza jumla ya mechi 20 na kufunga mabao manane kama mshambuliaji akishinda mataji ya Kombe la Washindi na Kombe la UEFA, kabla ya kusaini Bilbao ambako alicheza kwa miaka sita.
Uteuzi wake wa sasa unatimiza ndoto za pande zote mbili kufanya kazi pamoja, kwani ndiye aliyekuwa chaguo halisi wakati Tata Martino anaondoka Barcelona mwaka 2014, lakini ghafla Barca ikamgeukia Enrique.
Mwanzoni mwa msimu wakati Enrique alipoiambia bodi ya Barcelona hataongeza mkataba mwishoni mwa msimu, wakamuambia Valverde asiongeze mkataba Athletic Bilbao ili ahamie Nou Camp kiulaini.
Ametua na wasaidizi wake mwenyewe katika benchi la ufundi huku aliyekuwa Msaidizi wa Enrique namba mbili, Juan Carlos Unzue akihamia Celta Vigo na Jon Aspiazu akiwa msaidizi wa Valverde. 
Amejiunga akitokea Bilbao kama kocha wa mazoezi ya viungo, Jose Antonio Pozanco.
Hii si mara ya kwanza kwa Valverde kufanya kazi mjini Barcelona, kwa sababu aliifundisha Espanyol kuanzia mwaka 2006 hadi 2008 ambako aliiwezesha klabu kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la UEFA.
Kisha baadaye akashinda mataji matatu ya ligi na vikombe viwili akiwa na Olympiacos nchini Ugiriki.

Jumanne, 28 Februari 2017

BATULI AMPINGA WEMA, ‘WASANII TULIOSHIRIKI KAMPENI ZA CCM TULILIPWA NA MIKATABA IPO’

Msanii wa Filamu nchini, Batuli aliyeshiriki kampeni ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya ‘Mama ongea na Mwanao’ amekanusha taarifa zinazoeleza kuwa wasanii walioshiriki kampeni hiyo hawakulipwa.Batuli amesema taarifa hizo siyo za kweli na kueleza kuwa CCM iliwalipa wasanii wote walioshiriki katika kampeni ya ‘Mama Ongea na Mwanao’ na mikataba ya malipo hayo ipo.

 Nakanusha  za kwamba wasanii tulioshiriki kampeni za CCM ‘Mama ongea na mwanao’ hatukulipwa, tulilipwa na mikataba ipo” amesema Batuli
 Batuli amesema hayo leo Februari 28, 2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari, kufuatia taarifa ya msanii wa filamu, Wema Sepetu kuwa wanaidai CCM fedha za kampeni. Wema alinukuliwa akiongea hayo wakati akitangaza kujiengua katika chama hicho na kuhamia Chadema.
 Batuli amesema kuwa haiwezekani msanii mkubwa hivyo asema hakulipwa wakati yeye ndio alikuwa anawalipa wasanii wengine.Haiwezekani wewe staa mkubwa unasema haujalipwa, wakati wewe ndio ulikuwa unalipa watu” amesema Batuli

TETESI ZA USAJILI ULAYA 27.2.2017

TETESI ZA USAJILI ULAYA 27.2.2017

  • Arsenal wanamtaka kinda wa Manchester City Jadon Sancho, dogo huyo alisajiliwa kutokea Watford mwaka 2015 kwasasa yupo  katika Academy ya Manchester City. Moja kati ya Scout wa wachezaji wa Arsenal Rowley amekuwa akikomaa kuhakikisha wanamasa dogo ( The Sun)
  • Image result for hector bellerin
  • Hector Bellarin amesema kama ataondoka Arsenal ataelekea zake Manchester City kauli inakuja mara baada ya Barcelona kusema watasajili mchezaji kutoka kwenye academy yao kwa nafasi ya beki wa kulia, Bellarin alisema kama Wenger ataondoka basi naye atarudi zake Barcelon (Daily Star)
  • Everton wanaamini watawazidi Chelsea katika Issue ya kumsajili beki wa kati raia wa Uingereza Michael Keane majira ya Kiangazi, Everton wanamtaka wakati huo huo Chelsea wanamkodolea Macho (The Sun)
  • Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa anajipanga kuongeza wachezaji wawili mpaka watatu tu katika usajili wa majira ya joto (Independent