Pages

Ijumaa, 30 Desemba 2016

Alikiba ashinda tuzo ya Soundcity MVP 2016

Majina ya washindi wa tuzo za Soundcity MVP 2016 yametangazwa kwenye ukumbi wa Eko Hotel jijini Lagos, Alhamisi hii.
Jumla ya washindi 14 walitajwa kati ya washiriki 109 waliokuwa wakiwania tuzo hizo hapo mwanzo.

Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na wasanii wane akiwemo Diamond, Vanessa Mdee, Alikiba na Navy Kenzo.
Hatimaye Alikiba aliyekuwa wekwa kwenye kipengele kimoja amefanikiwa kuibuka na tuzo hiyo ya VIDEO OF THE YEAR kupitia wimbo wake wa Aje.

Sauti Sol wamefanikiwa kushinda tuzo ya BEST GROUP huku Wizkid alifanikiwa kuibuka na tuzo kubwa ya AFRICAN ARTIST OF THE YEAR

0 maoni:

Chapisha Maoni