Mchezaji wa klabu ya Everton, Yannick Bolasie anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti mwaka ujao.
Bolasei ambaye ni raia wa DR Congo, mwenye umri wa miaka 27 alipata majeraha wakati wa mechi kati ya Everton na Manchester United tarehe 4 mwezi huu.
Kocha wa Everton Rodald Koemen anasema kuwa mchezaji huyo alifanyiwa upasuaji wa kano za goti siku ya Alhamis kwa sasa anahitaji muda wa hadi majuma 10 ili kuweza kufanyiwa upasuaji wa pili.
Bolasie ambaye alijunga Everton kutoka Crystal Palace mwezi Agosti atakaa benchi kwa muda mrefu na hatachezakatika mechi ya kwanza ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon ambayo yataanza mwezi ujao.
0 maoni:
Chapisha Maoni