Msanii wa muziki Mwasiti Almas amesema ndani ya muda mchache toka apate
management ya kumsimamia tayari ameshaanza kuona mabadiliko makubwa
katika muziki wake.
Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Kaa Nao’ hivi karibuni, amedai ameanza kuona mabadiliko katika namna ambavyo nyimbo zake zinasambazwa.
“Kesema kweli sasa hivi maisha ya muziki wangu yamebadilika sana kusema kweli ndani ya muda mfupi, tayari naona management yangu inafanya kazi yake ipasavyo. Mimi sikuwahi kuwa na management serious kama hii kusema kweli mpaka napangiwa vitu vya kufanya usiende kule fanya hivi hii ni dalili nzuri kwamba wapo serious,”
Pia muimbaji huyo amedai ameamua kuachia audio ya wimbo wake kwanza tofauti na wasanii wengine wanavyofanya ili audio ipate nafasi yake na video ipate nafasi yake.
0 maoni:
Chapisha Maoni