Mohammad Ali
Barua iliyowekwa sahihi na mwanamasumbwi Mohammad Ali na kuandikiwa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, akitoa rambu ramba zake kufuatia kuawa kwa mtu aliyekuwa akipinga ubaguizi wa rangi imeuzwa kwa pauni 7,200.
Barua hiyo ilipewa chapa cha msaidizi wa meneja wa hoteli ya Elangeni iliyo mjini Durban ambapo Ali alikuwa akiishi wakati huo.
Barua hiyo iliyouzwa kwa mnunuzi kutoka nchini Marekania ilitarajiwa kuuzwa kwa kati ya dola 6,000 na 8,000.
CHRIS HANI
Muhammad Ali alikuwa nchini Afrika Kisini kwa kipindi kifupi mwezi Aprili mwaka 1993 baada ya kuwasili muda mfupi baada ya kuuliwa kwa Chris Hani tarehe 10 mwezi Aprili.
Hani alikuwa kamanda wa kundi la Umkhonto We Sizwe, kundi lililojihami la ANC Alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya ubaguzi wa rangi.
0 maoni:
Chapisha Maoni