Rais mteule wa Marekani Donald Trump
,amesema kuwa Marekani inafaa kuiomba China kuiweka manuwari ya
Marekani iliopatikana katika bahari ya kusini mwa taifa hilo.
China iliichukua manuwari hiyo katika pwani ya Ufilipino wakati meli za wanamaji wa Marekani zilipojaribu kuichukua, hatua ilioikasirisha Marekani.
China imesema kuwa itaikabidhi Marekani, lakini matamshi ya Trump huenda yakatatiza mpango huo.
Hii ni mara ya tatu katika wiki kadhaa kwa yeye kukosana na China.
Wakati huohuo Trump amekamilisha ziara yake ya wiki tatu ya kusherehekea ushindi , katika mji ulioshuhudia mkutano mkubwa zaidi wakati wa kampeni zake.
chanzo- BBC
0 maoni:
Chapisha Maoni