Mshambuliaji fundi wa klabu ya wenkundu wa Msimbazi Simba SC
inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, Ibrahim Ajibu, ameondoka klabuni
hapo na kutimkia nchini Msri kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo awali zilidai kuwa Ajibu ameondoka
bila kutoa taarifa kwa uongozi wa klabu, lakini baadaye meneja wa timu
hiyo Musa Hassan Mgosi amethibisha kuwa uongozi una taarifa na umetoa
baraka kwa mchezaji huyo kwenda kutafuta nje ya Tanzania.
“Ajibu kaenda Misri kwajili ya majaribio na kapata ruksa ya viongozi
kama ilivyo ada ya klabu ya Simba, Simba haimzuii mchezaji wake akipata
timu ya nje” Amesema Mgosi.
Ingawa Mgosi amesita kutaja timu ambayo Ajibu anakwenda, lakini
taarifa zinaeleza kuwa anakwenda katika timu ya Harass El Hadood.
0 maoni:
Chapisha Maoni