"Vikosi vya kijeshi viko tayari kuwapa watu matakwa yao, ikiwa wapatanishi wanaoongozwa na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari watashindwa kumshawishi bwana Jammeh kuachia madaraka, alisema Marcel Alain de Souza.
Ameongeza kuwa si matarajio ya Ecowas kuwasha moto eneo hilo na ikiwa bwana Jammeh anapednma watu wake, anahitaji kuondoka madarakani.
Awali Jammeh alikubali kushindwa na mfanyabiashara Adama Barrow wakati wa uchaguzi wa Disemba Mosi, lakini baadaye akaagiza kubadilishwa kwa matokeo akidai kuwa kulikuw na udanganyifu.
CHANZO -BBC
0 maoni:
Chapisha Maoni