Mwandishi Alex Mwenda
JAMANI
MIE UKAHABA SASA BASI ni Hadithi inayomuhusu binti wa kitanzania alietunukiwa
uzuri wa asili na mvuto wa kipekee aliojaaliwa na mungu ama hakika uzuri
aliokuwa nao ulikuwa ni kishawishi tosha kwa mwanaume yoyote aliemtazama binti
huyu na kutamani kuwa nae kutokana na mvuto aliokuwa nao binti huyu anaitwa
Jenifer na amezaliwa katika familia duni ya Mr. Brown na Mrs. Brown yenye watoto
watatu (3).
Ambao ni Peter, Joseph na Jenifer na katika watoto hawa watatu
mwanamke alikua ni Jenifer peke yake na ndie alikua mtoto wa kwanza kuzaliwa
katika familia hii yenye watoto watatu ambapo Peter na Joseph walikua ni wadogo
zake na Jenifer na walikuwa bado ni wadogo sana.
Na wazazi wa Jenifer Mr. Brown
na Mrs. Brown walitokea kumpenda sana binti yao Jenifer kwani ndio mtoto pekee
wa kike hivyo walionesha upendo mwingi kwa binti yao kwa kumtimizia mahitaj
yote muhimu na kumpa kila alichokitaka binti yao ili wamridhishe na kuhakikisha
wanampa malezi bora na kujenga upendo imara kwa binti yao. Kutokana na hali ya
ngumu ya maisha iliyokuwepo katika familia hiyo ya Mr. Brown na Mrs. Brown,
wazazi hawa walikaa na kujadili njia sahihi ya kuweza kukabiliana na umasikini
walio nao na kuweza kujikwamua kimaisha wakapata wazo la kumpeleka shule binti
yao Jenifer ili hapo baadae aje kuwasaidia wazazi wake kupitia elimu
atakayoipata shule hivyo wazazi wakakubaliana na kuanza mipango ya
kumuandikisha shule binti yao ili aanze kusoma, wazazi wa Jenifer walijitahidi
kutafuta pesa kwa hali na mali ikapelekea wazazi wa Jenifer kujiunga na kampuni
zinazotoa mikopo ya fedha lengo kupata pesa waweze kumtimizia mahitaji binti
yao aweze kuanza shule.
Mungu alileta kheri kwa wazazi hao na kufanikisha
kuipata pesa ya kumpatia binti yao kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya shule
na binti yao akafanikiwa kuanza elimu ya msingi akasoma darasa la kwanza mpaka
darasa la saba lakini alipo maliza darasa la saba matokeo yake hayakua mazuri
hivyo hakuweza kuchaguliwa katika shule za serekali kwa ajili ya kuendelea na
elimu ya sekondari lakini wazazi wa Jenifer hawakukata tamaa na waliendelea
kuwa na moyo wa kumsaidia binti yao Jenifer kwa vyovyote vile mpaka waone
mwisho wake kwani malengo yao binti yao asome mpaka daraja la juu afike mpaka
chuo kikuu,
baada ya Jenifer kumaliza elimu ya msingi na hakufanikiwa kufanya
vizuri katika mitihani yake ikabidi wazazi wajipange upya kutafuta ada ya
kumlipia binti yao ili aweze kujiunga na elimu ya sekondari kwa dhumuni la
kuhakikisha binti yao Jenifer anaendelea na elimu. Mungu hakuitupa familia hii
ya Mr na Mrs. Brown aliwajaalia wakafanikiwa kuipata pesa ya kumlipia ada binti
yao na wakamuandikisha katika shule ya kulipia ya sekondari iliyofahamika kwa
jina la
"GARDEN SECONDARY SCHOOL" Jenifer alijiun
ga na shule hii na kuanza elimu yake ya sekondari lakini kama ilivyo kwa vijana wengi wa kisasa kutofahamu umuhimu wa elimu na kushindwa kujua nini wanapaswa kukifanya pindi wanapo kuwa shule ndivyo ilivyokuwa kwa Jenifer. Jenifer hakujua umuhimu wa elimu na hakuona juhudi za wazazi wake kwake za kutafuta pesa kwa ajili ya kumlipia ada ili aje kuwasaidia baadae na kuwasaidia wadogo zake Peter na Joseph.
Kipindi Jenifer alipokua shuleni hapo akiendelea na elimu ya sekondari tabia yake ilibadilika akawa anautumia muda wake mwingi wa shule kujichanganya na marafiki ambao hawakuwa na msaada mzuri kwake na wakati mwingine alikua akiaga kwao anakwenda shule lakini alikua hafiki shule alikua anakwenda kwa marafiki anashinda na kurudi nyumbani wazazi wake hawakujua kinachoendelea kwa binti yao. Wakati mwingine Jenifer alikuwa ni mtu wa kupenda sana kwenda kwenye kumbi mbali mbali za starehe wakati alikua anatoka nyumbani kwao usiku akiwaaga wazazi wake kuwa anakwenda kwa marafiki zake anaosoma nao wanakwenda kukesha wakisoma na kujadiliana yale waliyofundishwa shuleni,
wazazi wa Jenifer hawakuwa na kipingamizi kwa binti yao walikua ridhwaa kukubaliana na kila anachohitaji binti yao ili mradi kumridhisha na kumfanya awe huru ili mwisho wa siku aweze kutimiza ndoto za wazazi wake hivyo wazazi walikua wakimpa ruhusa binti yao atoke usiku wakidhani anaenda kusoma na wenzake kumbe Jenifer alikua anatumia muda huo kutoka na kwenda CLUB (kumbi za starehe) na marafiki zake wanaenda kujirusha
na alikua anarudi nyumbani kwao kesho yake asubuhi, na ilikua kila ikifika siku ya Ijumaa mosi ndio anatoka usiku na wenzake, siku moja kama kawaida yake Jenifer na wenzake wametoka na kwenda kwenye kumbi za starehe huku nyumbani wazazi wanajua watoto wao wameenda katika masomo yao kama ilivyozoeleka, kipindi wapo CLUB kuna mwalimu wao wa shule alikuwepo katika ukumbi huo wa starehe na akakutana na kundi hili la wakina dada kama wanne akiwemo na Jenifer wakiwa wamevaa mavazi mafupi ya ajabu kama machangudoa wanaojiuza,
yule mwalimu wao alichokifanya akawaita kisha akawaambia "NAOMBA SIKU YA IJUMAA TATU MKIFIKA SHULE CHA KWANZA NAOMBA NIWAKUTE OFISINI KWANGU KAMA MLIVYO WANNE TENA MJE MKIWA MMEVAA HIZI NGUO MLIZO ZIVAA NA KILA MMOJA WENU AJE NA MZAZI WAKE" kisha mwalimu akawaambia wawe huru waendelee na mambo yao ila ikifika siku ya Ijumaa tatu siku ya shule wafanye kama alivyo agiza mwalimu huyo pale pale Jenifer na wenzake wakakosa amani na mudi ya kuendelea kufurahi usiku ule ikatoweka na kila mmoja wao akawa anawaza itakuaje hiyo siku ya Ijumaa tatu na wataanzia wapi kuwaeleza wazazi wao juu ya kosa hili walilofanya mpaka wamekutana na mwalimu kawaomba waende shule na wazazi wao.....?!
ITAENDELEA USIKOSE
0 maoni:
Chapisha Maoni