Na Alex Mwenda
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limekiri kupokea taarifa za
kutelekezwa kwa mtoto katika Hospitali ya Mkoa na mama aliyefahamika kwa majina
ya Neema Mwita na Magreth Maige mwenyeji wa Musoma, Mwenye umri wa miaka 17.
Akizungumza na mtandao huu kamishina msaidizi wa Jeshi la
Polisi Zuberi Mwombeji amesema sababu za Magreth kufanya kitendo hicho ni
kukosa uwezo wa kumuhudumia mwanae, lakini taarifa za awali walizokuwa nazo
jeshi la Police mama huyo alikuwa na kesi ya kubakwa na mchungaji.
Kamanda huyo amesema uchunguzi wa kisa cha kubakwa ulifanywa
na Jeshi la Polisi na haikuweza kuthibitika kuwa mchungaji ndiye aliyemfanyia
tendo hilo, na kuahidi kuwa Jeshi hilo litaendelea na uchunguzi zaidi wa kesi
hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni