Pages

Alhamisi, 22 Desemba 2016

KENYA- WABUNGE WADAIWA KUTWANGANA

Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira katika mji mkuu wa Nairobi, wakisema kuwa baadhi yao walinyanyaswa bungeni mapema asubuhi.

Kikao hicho maalum ambacho vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia kilitarajiwa kupigia kura marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambayo inaruhusu kuhesabiwa kwa kura moja baada ya nyengine katika uchaguzi wa urais mwaka ujao.

Serikali inataka mfumo ambao utasaidia shughuli ya kuhesabu kura iwapo mfumo wa kielektroniki utafeli lakini upinzani unasema kuwa ni njia moja ya kuiba kura.

Awali hatua ya kuupigia kura mswada huo ili ufanyiwe marekebisho ilisababisha kuzuka kwa ghasia siku ya Jumanne.

Upinzani wa CORD umesema kuwa mmoja ya wabunge wake alivuja damu usoni kufuatia mgogoro na wabunge wa chama tawala mapema siku ya Jumatano.

Cord imeenda mahakamani ikitaka marekabisho hayo kutopitishwa bungeni lakini chama tawala kimepitisha marekebisho hayo.

0 maoni:

Chapisha Maoni