Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha kwa umoja wao
wamegoma kwenda ziara ya Waziri wa Ardhi William Lukuvi na badala yake
wameelekea kituo cha polisi USA River kuhakikisha mwandishi mwenzao wa
ITV Halfan Liundi anaachiwa huru.
Katika hilo, azimio lililopitishwa ni kuwa wote kwa umoja wao
watamtenga mwandishi yoyote atakayehudhuria na kuandika kilichojiri
kwenye mkutano huo wa Lukuvi. Lihundi aliwekwa ndani na Mkuu wa Wilaya
ya Arumeru, Alexander Mnyeti akimtuhumu kuripoti taarifa ya maji ambayo
hakuipenda na kuwa ilikuwa ni habari ya uchochezi.
CHANZO: MTANZANIA
0 maoni:
Chapisha Maoni