Pages

Jumanne, 27 Desemba 2016

Kocha wa zamani wa Man United achaguliwa kuifundisha KRC Genk ya Samatta

 Image result for Albert Stuivenberg
Klabu ya soka ya KRC Genk ya Ubelgiji, imemtangaza kocha wa zamani wa Manchester United Albert Stuivenberg kuwa kocha mpya atakayeifundisha timu hiyo.
Image result for Albert Stuivenberg

Stuivenberg aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Louis Van Gaal kwenye timu ya United kwa misimu miwili kuanzia 2014 mpaka Juni 2016 na kufanikiwa kushinda kombe la FA msimu uliopita. Kocha huyo ambaye ni raia wa Uholanzi anachukuwa mikoba ya kuifundisha timu hiyo kutoka kwa Peter Maes ambaye ametimuliwa kutokana na kuwa na matokeo mabaya kwenye timu hiyo.

0 maoni:

Chapisha Maoni