YAWEZEKANA
kuwa ni mada ambayo imekuachahoi mpenzi msomaji wangu huku
ukijiuliza kama ni kweli zipo faida kwa watu wanaopendana
kwa dhati kununiana.
Faida
ipi hiyo zaidi ya maumivu na mateso ya moyo? Jamani ni
kweli kabisa kwamba kuna maumivu na karaha nyingi
unaponuniana na mpenzi wako, lakini wakati huo huo kuna
faida nyingi za kununiana naye. Mapenzi yana wigo mpana mno
ambao mtu anapaswa kuuangalia kwa jicho pana na akili
pembuzi kabla ya kuingia,namaanisha kwamba ni lazima
kuchunguza kina cha maji kabla ya kuzamia. Sasa basi,
zifuatazo ni faida tano utakazozipata ukiwa umenuniana na
mpenzi wako.
1. HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO
Ni
ukweli usiopingika kuwa, katika hali ya kawaida, ukiwa
mbali na mtu fulani katika jamii unayoishi ni vigumu
sanakujikuta umekwaruzana naye. Hii ni kwasababu utakuwa
hauingiliani nayekatika mizunguko yako, vivyo hivyo kwa
wapenzi walionuniana.Hali hii hupunguza kabisamigogoro ya
hapa na pale, kwani hiki ni kipindi ambacho mtakuwa
mbalimbali jambo ambalo huepusha maudhi ya
kibinadamu.Mfano, yawezakana katika kipindi mlichonuniana
na mpenziwako, uliingia ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake
kutoka kwa mtu aliyekosea namba. Kwa kuwa hauko naye karibu
jambo hili halitakuumiza maana hutaelewa nini kimeendelea
tofauti na kama ungelikuwa naye karibu.Kwa hiyo kuna baadhi
ya maumivu na maudhi ambayo utaepukana nayokwa kipindi cha
kununiana kwenu. Ni kweli kabisa kwamba hupunguza migogoro
na mitafaruku ya hapa na pale, umeelewa mpenzi msomaji
wangu? Haya twende kwenye faida ya pili.
2. KUBAINI TABIA X ZA MWENZAKO
Hiki
ni kipindi ambacho sasa kitakusaidia wewe kubaini tabia na
mienendo mibaya ya mwenzi wako. Hii ni kwa kuwa utakuwa
mbali naye hivyo naye hujiona kuwa yuko huru kufanya jambo
lolote analoona kuwa linafaa bila kujali uwepo wako kwani
kila mtu ana 'time' na mwenzake.Kama kuna asili ya maisha
yake ambayo aliiacha baada ya kuingia katika uhusiano na
wewe,ambayo ni mbaya zaidi sasa hapa ataanza kuirudia kwa
kujiona kuwa hana mtu wa kumzuia na kumbana.Kama ni mlevi
kupindukia,mchafu, muongo na tabia nyingine mbaya za
kufanana na hizi basi ataanza kuzionesha katika kipindi
ambacho mmenuniana.
3. KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI
Hapa
naomba nieleweke vizuri kabisa kwamba, ninapoongelea suala
la kutafakari zaidi katika kipindi ambacho wewe hauna
maelewano mazurina mwenzi wako, namaanisha kuwa utapata
muda mzuri zaidi wa kutafakari penzi lenu kwa ujumla.Ni
kipindi kitachokuongoza wewe kuwa na uelewa wa ni aina gani
ya mpenzi uliyenaye. Kivipi? Ni kwamba, katika muda huu
mara nyingi utataka kupata suluhu ya kununiana kwenu,
lakini pia katika kutafuta suluhuhiyo utapata fursa ya
kutafakari kwa kina juu yapenzi lenu huku ukimpima mwezi
wako kwa mtazamo chanya.
4. KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE
Si
kila rafiki wa mwenza wako ana nia nzuri na uhusiano wenu
au anafurahia penzi lenu. Mathalani, labda wewe ni msichana
na pengine miongoni mwa rafiki zakekuna mmoja au wawili
ambao hutamani sana kupata penzi lako.Sasa katika kipindi
ambacho utakuwa umenuniana na mpenzi wako basi itakuwa ni
nafasi nzuri kwao kuitumia kunyunyizia sumu ya kumponda
huku wakikutamkia maneno ya kukushawishi, hivyo utakuwa
umeelewa ni aina gani ya marafiki alionao mwenzi wako.Hii
si kwa msichana tu, hata kwa wanamume kwani huenda kati ya
rafiki wa 'girlfriend' wako, kuna wanaokutamani, sasa
wakiona huna uhusiano mzuri na mpenzi wako, watatumia
nafasi hii kukuambia maneno ya uongo juu yake na kukuonesha
kila dalili za kukutaka.Hivyo utakuwa umefahamu ni aina
gani ya rafiki ambao mpenzi wako anao. Tambua kwamba,
marafiki wengi wana tabia zinazofanana.
5. KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO
Katika
kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi
alilonalo huyo mtu wako juu yako. Kwa mpenzi aliye na
hisiaza dhati kabisa kwako, katika kipindi hiki atakuwa ni
mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo lenu.Pamoja
na kwamba wewe utakuwa umenuna, bado yeye ataonesha
kukujali kama kawaida, atakupigia simu za hapa na pale
yaani ilimradi tu asikie angalau sauti yako,lengo lake
likiwa ni kutaka kurejesha ukaribu ambao sasa anaona kama
akiupoteza itakuwa ni maumivu kwake.Kwa mantiki hiyo basi,
utagundua ni kwa jinsi gani anathamini penzi lenu na ni
aina gani ya penzi alilonalo kwako. Yote haya utabahatika
kuyajua kupitia kipindi cha kununiana kwenu.Hata hivyo,
niwatahadharishe kwamba, kuandika haya isiwe ni tiketi ya
wewe sasa kuanza kununiana na mpenzi wako eti kwa kigezo
kwamba utapata nafasi ya kumfahamu, la hasha! Siku zote
katika uhusianowako epuka maudhi na migogoro isiyokuwa ya
maana.
BY CLEVER
0 maoni:
Chapisha Maoni