Pages

Jumatatu, 19 Desemba 2016

UGAIDI WATAJWA MAUWAJI YA BALOZI.

MSHAMBUIAJI 

Urusi imehusisha mauaji ya Balozi Karlov na ugaidi.Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Moscow amesema Uturuki wamehakikishiwa kwamba kutakuwa na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo na wote watakaokuwa wamehusika wataadhibiwa.

Meya wa Ankara amesema mauwaji hayo yamelenga huharibu mahusiano ya nchi hiyo na Urusi. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry amesema Marekani iko tayari kusaidia katika uchunguzi wa tukio hilo.                
                                                          BALOZI KARLOV
 

Balozi huyo alishambuliwa katika eneo la sanaa ya uchoraji katika mji mkuu wa Ankara.
Ripoti zinasema kuwa balozi huyo alikuwa akitoa hotuba wakati mtu aliyekuwa amejihami na bunduki alipompiga risasi na kutoa ujumbe kuhusu mji wa Aleppo nchini Syria.
Watu kadhaa wamejeruhiwa .



0 maoni:

Chapisha Maoni