Na Alex Mwenda, Songea
MKUU WA MKOA RUVUMA SIKIA KILIO NA OMBI HILI LA MAGHRET
ABAKWA NA MCHUNGAJI, APEWA VVU NA ATELEKEZWA NA MTOTO.
Ni msichana wa miaka 16 kwa mujibu wa maelezo yake! Anaeleza
kuwa alibakwa zaidi ya mara nane na Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mkuzo Maliasili
Mjini Songea.
Msichana Magret Mgena ameeleza kuwa yeye ni mwenyeji wa Mkoa
wa Mara na alifika Mkoani Ruvuma baada ya kuchukuliwa kufanya shughuli za
ndani.
Mchungaji huyo alimchukua Magret kutoka kwa aliokuwa
akiwatumikia kwa kuwatisha kwamba angeliwafunga kwani wamemtorosha binti huyo
kutoka kwao Musoma! Na yeye kwakua ni mchungaji alipenda aishi nae amlee! Kumbe
alikua na dhamira yake moyoni.
Magret anaeleza La hasha Mchungaji huyo Alikua akimfuata
chumbani nyakati za usiku na hata pale mkewe alipokuwa akisafiri kwenda masomo
na kumlazimisha tendo la ndoa.
Miezi kadhaa kupita Magret alijipata na Ujauzito! Mchungaji
alihisi ile hali na alimueleza asiseme kuwa yeye ndiye aliyempatia ujauzito
huo! Na alimueleza aseme ile mimba ni ya kijana waliyekuwa nae Mtaani! Binti
alifanya hivyo kwakua alikua na hofu tele.
Magret anaeleza kuwa mchungaji alisimama mbele ya kanisa na
hata mbele ya wazee wa kanisa na kusema binti huyu anapaswa kutueleza ninani
aliyempatia ujauzito! Kwani alihofu kwakua watu walijua yeye mchungaji ndiye
anaeishi na kwake na huenda watu wangelimuhisi yeye.
Mchungaji alimtelekeza Mtoto Magret! Magreti alifikishwa
Dawati la Jinsi na Watoto Mkoani Ruvuma Mchungaji aliahidi kupima DNA endapo
mtoto angezaliwa salama.
Mtoto Magreth alijifungua salama, na wakati wa Clini Mtoto
Magreth aligundulika kuwa na maambukizi ya virus vya ukimwi, anasema hakuwahi
kutembea na Mvulana yeyote maishani mwake kwani alizaliwa mwaka 2001.
Hospitali amepatiwa vidonge vya ARV anatumia, kazi hana!
Pesa ya chakula hana! Mahala pa kulala hana! Mtoto aliyejifungua ameamua
kumtelekeza Katika hospitali ya Mkoa Ruvuma kwakukosa kipato cha kujihudumia.
Mtoto Magreth sasa anahangaika mitaani OMBI lake kuu Anaomba
akutanishwe na Mkuu wa Mkoa Ruvuma ili Amueleza kisa hiki kwa huenda ndie akawa
mkombozi wake! Na zaidi anatamani kuona Sheria inachukua Mkondo wake.
Magreth amekosa matumaini na watu waliokuwa wakimsaidia
kwani hakuona hatua stahiki zikichuliwa dhidi ya Mchungaji huyo! Na yeye
amekwisha athirika na hana wakumsimami mbele za haki.
0 maoni:
Chapisha Maoni