Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetoa ratiba ya mechi za
awali za michuano ya klabu Afrika mwakani, Kombe la Shirikisho na Ligi
ya Mabingwa wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Ngaya de Mbe ya Comoro.
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam
FC wao wataanzia Raundi ya kwanza ambako watamenyana na mshindi kati ya
Mbabane Swallows ya Swaziland na Opara United ya Botswana.
Yanga wataanzia ugenini wikiendi ya Februari 10 hadi 12 kabla ya marudiano wikendi ya Februari 17 hadi 19, mwaka huu.
Azam wao wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 na marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.
Yanga wakivuka hatua hiyo watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya
Zambia na APR ya Rwanda katika Raundi ya kwanza. Na Yanga wataanzia
nyumbani Machi 10 hadi 12 kabla ya marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani,
2017.
0 maoni:
Chapisha Maoni