Rapa Darassa baada ya kunusurika kifo katika ajali mbaya ya gari akiwa
na muongozaji wa video nchini Hanscana huko Kahama, Jamatano hii alienda
katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwaajili ya kucheki
afya yake.
Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii akiwa
hospitalini hapo, Darassa alisema aliamua kwenda kucheki afya yake baada
ya kuwa na maumivu ya kichwa yaliyotokana na ajali hiyo.
“Nipo hospitalini Muhimbili sasa hivi nawashukuru sana madaktari wa
hapa wamenipokea vizuri wamenipa huduma nzuri sana,” alisema Darassa.
“Wamenicheki kwa sababu nilikuwa najisikia vibaya sana sehemu za
kichwani nashukuru Mungu majibu yanaonyesha kila kitu kipo poa kabisa
kuna damage ndogo wanaifanyia kazi naendelea na matibabu ila
nimeshauriwa kupunguza mizunguko kwa wiki moja ili niweze kupumzika na
kutibu hayo maumivu ya kichwa,”
Darassa na Hanscana pamoja na wenzao wawili alipata ajali hiyo wakati
wakiwa njiani wakitokea Kahama mkoani Shinyanga kwenda Kakola mkoani
humo kwaajili ya show.
0 maoni:
Chapisha Maoni