Pages

Jumatatu, 19 Desemba 2016

SIKO TAYARI KUTOA ALBAMU KWA SASA-MWANA FA


Image result for MWANA FA
Mwana FA amedai kuwa hadi pale patakapotokea uwekezaji wa kueleweka kwenye biashara ya usambazaji wa album nchini, ndipo atakapofikiria kutoa ya kwake.
Akiongea na mtangazaji wa Mashujaa FM, Baby Dinny, FA amedai kuwa kutoa album katika mazingira ya sasa ni kujitakia hasara kubwa.
“Sio kwamba kwasababu watu wanataka album basi lazima wapate hata kama ni kwa gharama yako, hata kama ni kwa kupata hasara,” amesema FA.
“Kwahiyo tunapokwama ni kwenye distributors, hatuna watu wa kuaminika, hatuna makampuni ya kueleweka ambayo yanaweza yakafikisha muziki nchi nzima na kuhakikisha msanii anapata angalau nusu ya anachostahili,” ameongeza.
Hitmaker huyo wa Dume Suruali, amedai kuwa album ya mwisho kutoa ilikuwa ni Habari Ndio Hiyo aliyoshirikiana na AY ambayo anadai haikuwapa faida yoyote licha ya kuwa kubwa na iliyowatumia nguvu na muda mwingi kuiandaa.

0 maoni:

Chapisha Maoni