Zaidi
ya watu 21,000 katika halmashauri
ya manispaa ya songea mkoani Ruvuma
wanaishi na virus vya ukimwi .
Hayo
yamesemwa na afisa habari manispaa ya songea albano midello na kubainisha kuwa
takwimu toka kitengo cha uratibu wa ukimwi na tiba katika manispaa ya
songea zinaonyesha kati ya watu wenye
virus ,watu zaidi ya 10,000 ndiyo wanaugua ugonjwa wa ukimwi.
Midelo
amesema pia idadi hiyo ya wagonjwa ndio wanaotumia dawa za ARV na kwamba
maambukizi ya virus vya ukimwi katika manispaa ya songea ni asilimia nne ,na
amezitaja kata zinazoongoza kwa maambukizi kuwa ni bombambili,mateka,Ruvuma na
lilambo.
Afisa
habari huyo amebainisha kuwa takwimu za maambukizi ya virus vya ukimwi katika
manispaa ya songea kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi desemba 2015
zinaonyesha kuwa watu 319 wamegundulika kuwa na maambukizi mapya ya virus vya
ukimwi
0 maoni:
Chapisha Maoni