Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba weekend
hii alimtembelea mama Chidi Benz na kufanya naye mazungumzo ili
kuangalia namna ya kumsaidia rapa huyo pamoja na kuongeza kasi ya
kupambana na magenge ya wauzaji wa Madawa ya kulevya.
Hatua hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita katika mitandao ya kijamii
kuzagaa picha za rapa huyo akiwa katika hali mbaya iliyosababishwa na
matumizi ya Madawa ya kulevya.
Waziri huyo baada ya kumtembelea mama Chidi Benz, kupitia instagram aliandika.
Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo “Chid Benz” ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya.Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola.
Mbali ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo,ni wajibu wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida.
Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa,unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya
0 maoni:
Chapisha Maoni