Takriban watu 39
wakiwemo wageni 15 wanahofiwa kuuawa katika shambulio la klabu ya
burudani mjini Istanbul Uturuki, kulingana na waziri wa maswala ya
ndani nchini humo.
Mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki
aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakijiburudisha katika mkahawa huo
wa Reina saa saba usiku wakati ambapo watu walikuwa wakisherehekea
kuingia kwa mwaka mpya.
Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya
kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza
kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.
Baadhi yao iliwabidi kujirusha baharini kuepuka msusuru wa risasi zilizokuwa zinafyatulia.
Polisi mmoja ni miongoni mwa waliofariki.
Huku waliojeruhiwa wakikimbizwa hospitali, maafisa
wa usalama wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo lakini muhusika
wa shambilo hilo hajakamatwa bado.
0 maoni:
Chapisha Maoni