Maafisa nchini Brazil wanasema wafungwa 55 wamepoteza maisha katika vurugu zilizotokea katika gereza nje ya mji wa Manaus.
Baadhi ya miili imekatwa vichwa huku mingine ikiwa imechomwa moto.
Mkuu wa usalama katika jimbo la Amazonas, Sergio Fontes, amewaambia waandishi wa habari kuwa vurugu hizo zilikuwa zimepangwa muda mrefu.
"kila kitu kinaashiria kwamba vurugu zilizotokea zilikuwa zimepangwa muda mrefu.
Wafungwa waliweka bayana kwa uongozi wa gereza kwamba kila kitu kitakuwa sawa katika msimu huu wa sikukuu.
Hawakutekeleza ahadi yao, lakini huwezi kuwaamini wahalifu?"
Fontes ameongeza kusema kuwa baadhi ya wafungwa walitoroka na wengine wameuawa.
Hata hivyo, Idadi kubwa ya wafungwa waliokuwa wametoroka tayari wamekamatwa.
Nako nje ya gereza, ndugu wa wafungwa waliokusanyika walijawa na shauku ya kutaka kujua hali ya ndugu zao.
Maafisa wa gereza wanasema makundi hasimu yaliyopo nje na ndani ya gereza yamepigana kwa kutaka kuwa na sauti dhidi ya kundi jingine.
Wajumbe wa moja wapo ya makundi hayo, wametengwa katika magereza mengine.
Nae waziri wa katiba amekwenda katika gereza hilo ili kuangalia uwezekano wa kuhamishwa kwa baadhi ya wafungwa katika gereza jengine
0 maoni:
Chapisha Maoni