Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemkana kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya West Ham Utd Dimitri Payet.
Wenger amemkana kiungo huyo, baada ya kuhusishwa na taarifa za
kuwindwa na washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal),
katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
Mzee huyo kutoka nchini Ufaransa alikanusha taarifa za kuwa katika
mpango wa kumsajili payet, alipokutana na waandishi wa habari jana
katika mkutano maalum uliokua unazungumzia mchezo wa ligi kuu ya soka
nchini England wa mwishoni mwa juma hili, ambapo The Gunners
watapapatuana na Burnley.
“Binafsi ni mshabiki mkubwa wa Payet kutokana na uwezo wake mzuri wa
kucheza soka, lakini sina mpango wa kumsajili kama ilivyoripotiwa na
baadhi ya waandishi wa habari ambao naamini ni miongoni mwenu,” Alisema
Wenger.
“Tuna wachezaji wengi ambao wana uwezo wa kucheza kama Payet, hivyo hakuna sababu ya kumsajili kwa sasa.”
Payet amekua kwenye shinikizo la kutaka auzwe katika kipindi hiki cha
dirisha dogo la usajili, na juma lililopita aligomea mazoezi, hali
ambayo ilisababisha aondolewe kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya
Crystal Palace.
0 maoni:
Chapisha Maoni