Pages

Alhamisi, 19 Januari 2017

Chipukizi wa Tanzania wasajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu Zambia na Kenya

Image result for Zanaco
Mabingwa wa Ligi Kuu Zambia, klabu ya Zanaco imemsajili mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, Ayubu Reuben Lyanga kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja.

Lyanga  mwenye umri wa miaka 20 ametokea klabu ya African Sports na amesajiliwa baada ya kufuzu majaribio yaliyohusisha wachezaji wachezaji kutoka Kongo na Afrika Magharibi chini ya aliyekuwa kocha mkuu,  Numba Mumamba ambaye kwa sasa amebadilishwa kuwa mkurugenzi wa ufundi.


Zanaco ni mabingwa mara saba wa Zambia na mwaka huu watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. Hata hivyo jina la Lyanga alijajumuishwa katika kikosi chao cha Ligi ya Mabingwa jambo linalowalazimu  Zanaco kulipa faini endapo wataongeza jina lake.

Wakati huo huo, kiungo mwingine chipukizi, Abdul Hilary  aliyekuwa akichezea African Lyon ameelekea nchini Kenya kukamilisha taratibu za kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu nchini humo, Tusker.
Hilary alifuzu majaribio

0 maoni:

Chapisha Maoni